Ijue Corona, kujikinga , dalili na hatua za kufuata

 

Utajilindaje na Corona virus (Covid 19).

Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya vyanzo vingi vya habari kutoa taarifa kuhusu kujikinga na Virusi vya Corona (Covid 19) imekuwa vizuri kwangu pia kukupa taarifa zote muhimu baada ya kufuatilia kwa kina mbinu za kujikinga, Madhara pamoja na athari zitokanazo na Corona katika lugha ya Kiswahili ili kuweza kupunguza janga hili kubwa kuleta madhara makubwa Afrika mashariki na Tanzania.

 

Unaweza kupunguza uwezekano wa kusambaa au kuathirika na Kirusi cha Corona (Covid 19) kama utatimiza yafuatayo:-

 • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa sabuni ya dawa au dawa maalumu (sanitizers) Dawa hizi zinapatikana katika gharama ya kuanzia 1,000 (Elfu moja) hadi 30,000.

 

 • Ziba mdomo na pua wakati kwa kupiga chafya au kukohoa kwa kutumia tissue (karatasi laini) au kwa kutumia kiwiko chako. Epuka kuziba kwa kutumia mkono ili kuwalinda wengine kupata Kirusi hicho.

 

 • Kukaa mbali na watu wenye mafua au dalili za mafua na kifua angalau mita moja.

 

 • Epuka kusalimiana kwa kushikana mikono hata kwa watu wako wa karibu.

 

 • Epuka kupeleka mkono karibu na pua, macho na mdomo bila kunawa mikono yako.

 

 • Epuka kuweka kushika simu na vifaa vyengine vya kieletroniki vya watu ambavyo muda mwingi vinakuwa vimeshikwa na watumiaji wake.

 

 • Tumia wipes (Vifutio maalumu vyenye dawa) kufuta simu au sehemu ya computer inayokubidi kushika kwa mikono yako au nawa mikono baada ya kushika sehemu hizo.

 

 • Unapopika nyama au mayai hakikisha yameiva vizuri.

 

 • Punguza ukaribu na watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata virusi vya Corona. Mfano Wazee, na watu wenye magonjwa sugu (Kisukari, Pressure and matatizo ya kupumua).

 

 • Jiepushe sehemu na sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu.

 

Corona inasambaaje?

 1. Kuwa karibu na mgonjwa wa Corona au mtu aliye na Corona kabla hajaanza kuonesha dalili.
 2. Kushika sehemu ambazo mgonjwa wa Corona kashika (Ambapo aliacha baadhi ya maji maji yanayotoka puani au baada ya kukohoa.)

 

 

Dalili zinazoweza kuonekana kwa mgonjwa mwenye virusi vya Corona ni kama zifuatazo.

 

 

 • Homa
 • Mafua na kikohozi kikavu
 • Kushindwa kupumua vizuri.

 

Hatua za kufuata ukijihisi una maambukizi ya Corona au ukiambukizwa Corona.

 • Nawa mikono yako kwa maji sabuni ya dawa

 

 • Epuka kuwahudimia watu wengine (kupikia, kuwasaidia wazee na kadhalika)

 

 • Vaa kitambaa maalumu(mask) Endapo huwezi kukaa mbali na watu hatarishi.

 

 • Jiweke mbali na wengine kupunguza uwezekano wa kusambaza Corona (self-quarantine)

 

 • Wahi kituo cha afya (hakikisha unaondoa uwezekano wa kuambukiza wengine wakati unaenda kituo cha afya)

 

Kumbuka: -

 • Hadi sasa haijapatikana dawa maalumu ya kujikinga au kutibu moja kwa moja mgonjwa wa Corona virus.
 • Fuata ushauri unaotolewa na shirika la afya duniani pamoja na mamlaka husika katika nchi yako dhidi ya kuzibiti na kupambana na Corona virus.
 • Fuatilia kwa umakini taarifa zote zitolewazo kuhusu Corona Virus.
 • Kuepuka taarifa za uongo fuatilia vyombo vya kuaminika katika mitandao.
 • Usisambaze taarifa usizo na uhakika nao.

 

 

Jitahidi kusambaza ujumbe huu kwa rafiki na watu wa karibu ili kuweza kuwaokoa na kuwalinda na Corona virus.

 

Nashukuru kwa kusoma nakala hii hadi mwisho, nitazidi kuhakikisha unapata taarifa zote muhimu kuhusu janga hili. Tafadhali endelea kufuatilia Blog hii ili kujua zaidi kuhusu corona. Ingawa blog haikuwa mahususi kwaajili ya mambo ya afya ila nimeona vyema kukusanya taarifa muhimu kuhusu korona ili ujue ukweli wote na uweze kujilinda wewe pamoja na wengine uwapendao.

 

Vyanzo vya Taarifa.

https://gulfnews.com/  ,  https://www.health.gov.au/ , https://www.express.co.uk/ , https://www.health.harvard.edu/